Uchumi wa Zambia unakua lakini yahitaji marekebisho ya sera- IMF

27 Machi 2017

Shirika la fedha duniani, IMF limesema Zambia imechukua hatua ili kuwezesha shirika hilo kusaidia mipango ya uchumi.

IMF imesema hayo kufuatia ziara ya wiki mbili nchini humo iliyoongozwa na Tsidi Tsikata.

Mathalani imetaja mipango hiyo kuwa ni pamoja na mipango ambamo kwayo inahakikisha fedha za umma zinatumika ipasavyo na kiuendelevu pamoja na malipo ya malimbikizo ya madeni ya umma bila kulundika mengine.

Bwana Tsikata amesema kwa hatua hizo, uchumi wa Zambia unatarajiwa kukua kidogo kwa asilimia 3.5 mwaka huu wa 2017.

Hata hivyo amesema ili kuendeleza ukuaji jumuishi wa uchumi, ni lazima Zambia itunge sera bora na ifanye marekebisho ya kiuchumi yanayowezesha ushindani.

Wakati wa ziara hiyo, ujumbe huo ulikuwa na mazungumzo na viongozi wa serikali ambapo walijadili uzoefu wa Zambia na mipango ya awali ya IMF ikiwemo ruzuku katika setka ya kilimo na nishati.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter