Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi Sudan Kusini zingatieni amani- Mahamat

Viongozi Sudan Kusini zingatieni amani- Mahamat

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Muungano wa Afrika, AU, Moussa Faki Mahamat yuko nchini Sudan Kusini ambako ametoa wito wa utekelezaji wa mkataba wa amani ili kumaliza machungu yanayokabili wananchi.

Akizungumza huko Ganyiel, kwenye jimbo la Unity Kusini, Bwana Mahamat amesema kiwango cha machungu ni cha kupitiliza na zaidi ya yote janga la kibinadamu.

Amesema aliguswa na kile alichoshuhudia na kutoa wito kwa pande husika katika mzozo kuhakikisha kuna amani ili taifa hilo liweze kurejea katika hali ya kawaida.

Kabla ya kwenda Sudan Kusini, mwenyekiti huyo wa kamisheni ya AU alikwenda Nairobi, Kenya ambako alihudhuria kikao maalum cha viongozi wa IGAD kuhusu wakimbizi wa Somalia.