Tukiwakumbuka wanaoshikiliwa au kutoweka, tunaimarisha ulinzi kwa wafanyakazi:UM

25 Machi 2017

[caption id="attachment_313458" align="alignleft" width="350"]wafanyakazium

Hadi kufikia Machi 15 mwaka 2015 wafanyakazi 33 wa Umoja wa Mataifa na wanaohusiana na Umoja huo wanashikiliwa na mamlaka za nchi 15. Mfanyakazi mmoja ametoweka na hajulikani haliko huku makandarasi wawili wa Umoja wa mataifa bodo wanashikiliwa na waliowateka nyara.

Siku ya kimataifa ya mshikamano na wafanyakazi wa Umoja wa mataifa wanaoshikiliwa au waliotoweka huadhimishwa kila mwaka Machi 25, katika siku ya kumkumbuka mwandishi wa habari Alec Collet aliyekuwa akifanya kazi na shirika la Umoja wa mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, wakati alipotekwa na mtu mwenye silaha 1985. Maiti yake hatimaye ilipatikana kwenye bonde la Bekaa Lebanon mwaka 2009.

Umoja wa Mataifa unasema katika miaka ya karibuni umechukua hatua muhimu hasa wakati mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa Umoja huo yakiongezeka.

Umeongeza kuwa siku hii ni ya kuchagiza hatua, kudai haki na kuimarisha juhudi za Umoja wa Mataifa kulinda wafanyakazi wake na walinda amani, pamoja na washirika wa Umoja huo katika jumuiya zisizo za kiserikali na wanahabari.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud