Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni azimio la kihistoria kulinda urithi wa dunia dhidi ya ugaidi

Ni azimio la kihistoria kulinda urithi wa dunia dhidi ya ugaidi

[caption id="attachment_313389" align="aligncenter" width="625"]utamaduniga

Baaraza la usalama la Umoja wa mataifa Ijumaa limepitisha azimio la kihistoria kulinda urithi wa kitamaduni wa dunia dhidi ya makundi ya kigaidi wakati wa vita vya silaha.

Azimio hilo litashughulikia masuala muhimu ya usafirishaji haramu wa bidhaa za kitamaduni kama chanzo cha fedha za ufadhili wa ugaidi na pia linaweka bayana njia za kulinda urithi wa kitamaduni wakati wa vita ambako hali inakuwa tete.

Akizungumzia kupitishwa kwa azimio hilo mkurugenzi mtendaji wa ofisi ya umoja wa mataifa ya dawa na uhalifu UNODC bwan Yury Fedotov amesema bila shaka litaimarisha uwezo wa jumuiya ya kimataifa kushughulikia masuala hayo na pia ametoa wito wa ushirikiano zaidi

(FEDOTOV CUT)

Tunahitaji kutekeleza majukumu kwa uhakika zaidi na tunahitaji nchi wanachama kutoa msaada katika ari ya kushirikiana majukumu kwa nia ya kuweka bayana kuhusu ukubwa wa uhalifu huo ili kuisaidia jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za pamoja.

Naye mkurugenzi mkuu wa shirika la elimu sayansi na utamaduni UNESCO Bi Irina Bokova katika kikao hicho amesema utamaduni ndio kitambulisho cha mtu na ni muhimu ukalindwa

(SAUTI YA IRINA BOKOVA)

"Mabibi na mabwana, wajumbe wa baraza la usalama uridhi wa kitamaduni ndio utambulisho wetu, urithi wa kitamaduni utaeleza hadi ya watu wa kila aina na pia inabeba mila zinazounganisha ubinadamu wa pamoja, kila mahali ambako watu wanachoma vitabu na utamaduni wanaishia kuchoma binadamu wenzao. Uharibifu wa makusudi wa urithi ni uhalifu wa kivita na kupigania urithi wa kitamaduni ni zaidi ya suala la kitamaduni, ni suala la usalama ambalo haliwezi kutenganishwa na lile la kutetea uhai wa binadamu.”

Baraza la usalama limepitisha azimio hilo kufuatia mkutano kuhusu “ukarabati wa amani na usalama wa kimataifa: uharibifu na usafiorishaji haramu wa urithi wa kitamaduni unaofanywa na makundi ya kigaidi katika nyakati za vita vya silaha.