Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tatizo la kifua kikuu bado ni changamoto duniani-WHO

Tatizo la kifua kikuu bado ni changamoto duniani-WHO

Ugonjwa wa kifua kikuu au TB bado ni changamoto kubwa duniani na kwa kulitambua hilo shirika la afya ulimwenguni limetoa muongozo mpya wa kimaadili likiadhimisha siku ya kifua kikuu ambayo hua Machi 24 kila mwaka. Flora Nducha na taarifa kamili.

(TAARIFA YA FLORA)

Baadhi ya mambo yaliyojumuishwa katika muongozo huo wa WHO ni masuala ya kutengwa kwa wagonjwa wa kuambukiza, haki ya wagonjwa wa kifua kikuu magerezani, na sera za kibaguzi dhidi ya wahamiaji walioathirika na TB.

Kauli mbiu mwaka huu ni “tuungane kutokomeza TB” lakini kuna baadhi ya nchi tatizo linazidi kuongezeka ikiwemo Tanzania kwa mujibu wa Dr Liberate Mleo meneja wa mpango wa taifa wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma nchini humo

(Sauti ya Dkt. Liberate)

Ameongeza kuwa makundi hatarishi ni kuanzia umri wa miaka 45 , maeneo ya vijijini, na vile vile kwa walioathirika na virusi vya ukimwi VVU, na anataja baadhi ya hatua zinachukuliwa kudhibiti hali hiyo

(Sauti ya Dkt. Liberate)

Katika video hii, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini Tanzania, Ummy Mwalimu alipotembelea wodi ya wagonjwa wa kifua kikuu kwenye hospitali ya Mount Meru mkoani Arusha hii leo.