Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mikopo yalenga kukwamua wanawake kiuchumi nchini Tanzania

Mikopo yalenga kukwamua wanawake kiuchumi nchini Tanzania

Umaskini uliokithiri umepunguzwa zaidi ya maradufu katika nchi mbali mbali duniani tangu mwaka 1990. Wakati hii ikiwa ni hatua kubwa, bado yaelezwa kuwa mtu mmoja kati ya watano katika nchi zinazoendelea anaishi kwa kutumia chini ya dola moja na senti ishirini na tano kila siku na kuna mamilioni wengi ambao wana kipato kidogo zaidi tu ya kiwango hicho huku kukiwa na hatari ya watu kutumbukia katika dimbwi la umaskini.

Katika kuhakikisha kwamba hakuna mtu atakayeachwa nyuma kuelekea mwaka 2030, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwemo Tanzania wameweka mikakati mashinani kama vile kuwapatia wananchi mikopo ili kuwakwamua kutoka katika lindi la umaskini. Je ni changamoto zipi zinazokabili utoaji wa mikopo kwa wanawake wajasiriamali? Basi ungana na Paulina Mpiwa wa redio washirika Sengerema redio ya Mwanza Tanzania.