Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwa kila uasi unaofanyika Sudan Kusini unachagiza kisasi-Guterres

Kwa kila uasi unaofanyika Sudan Kusini unachagiza kisasi-Guterres

Kwa kila mtoto anayekufa, kwa kila mwanamke au msichana anayebakwa na wahusika kukwepa sheria, na kwa kila mvulana anayeingizwa vitani na kulishwa dhana za chuuki , kumbuka kuna mzazi aliyejawa na gadhabu, mume au baba aliyeghubikwa na huzuni na kutumbukia katika kusaka ulipizaji kisasi.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kwenye mjadala wa baraza la usalama alhamisi kuhusu hali ya Sudan Kusini, na kuongeza kuwa mgogoro wa Sudan kusini unaendelea kuongeza madhila kwa mamilioni ya watu wa taifa hilo change.

Guterres amesema pande zote jeshi la serikali na upinzani wanaendeshaoperesheni za kijeshi katika maeneo kadhaa, zikiwa na athari kubwa kwa raia ambao wanakabiliwa na machafuko yasiyokwisha na kulazimishwa kuzihama nyumba zao.Na hivyo amesema ili kulirejesha taifa hilo katika hali ya amani na kukabili baa la njaa kuna malengo matatu muhimu lazima yafanyike mara moja

(Sauti ya Guterres)

“Mosi kufanikisha usitishaji uhasama mara moja, pili kufufua mchakato wa amani, hii ikimaanisha kuhakikisha uwakilishi na majadiliano na upinzani, asasi za kiraia na Wasudan wote bila kujali kabila, katika mpito na katika mapendekezo na mjadala wa kitaifa. Na tatu kuhakikisha hakuna vikwazo vya misaada ya kibinadamu, ikiwa ni pamoja na uhuru wa kutembea kwa UNMISS na kikozi cha ulinzi cha kikanda cha baadaye."

Ameongeza kuwa katika siku mbili zijazo wakuu wa IGAD watakutana Nairobi Kenya na amewataka wajumbe wa baraza la usalama na viongozi wa IGAD kwa kauali moja kuahidi kuunga mkono malengo hayo matatau na kushinikiza pande kinzani Sudan Kusini kuyatekeleza.

Kwani ameongeza kuwa ndoto zote zailizoambatana na kuzaliwa kwa taiafa la Sudan kusini sasa zimezimwa na migawanyiko ya ndani na tabia za kutowajibika kwa baadhi ya viongozi wa taiafa hilo.