Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maadhimisho ya Siku ya TB Duniani yasisahau wahamiaji-IOM

Maadhimisho ya Siku ya TB Duniani yasisahau wahamiaji-IOM

Tukielekea siku ya Kifua Kikuu Duniani, Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM imeungana na Shirika la Afya Duniani, WHO na washirika wengine kuongeza maradufu juhudi za uelewa wa umma kuhusu kifua kikuu ama TB na madhara yake kwa jamii zilizo hatarini zaidi kama vile wahamiaji.

IOM imesema ugonjwa huo ambao WHO imesema unatibika, husababisha unyanyapaa na ubaguzi katika nchi nyingi, na hivyo kupunguza fursa hususan kwa wahamiaji kupata huduma za kuutibu na kuuzuia ugonjwa huo.

liImeongeza kuwa moja ya makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa dunia katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu wakimbizi uliofanyika Septemba 2016 ni serikali na jumuiya za kimataifa kukuza upatikanaji wa huduma za afya na kuheshimu haki za kibinadamu kwa kundi hilo, jambo ambalo limesema bado linaleta wasiwasi mkubwa na linahitaji kushughulikiwa haraka.

Kwa mantiki hiyo, IOM pamoja na washirika wake wanatoa wito wa hatua za kimataifa na uratibu tarehe 24 Machi mwaka huu na kuendelea, kuhakikisha TB inatokomezwa naujumbe wake ni, "Ungana Kukomesha TB kwani TB haina mpaka na ni lazima tuhakikishe kuwa "Hakuna Anaeachwa Nyuma".