Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna changamoto lakini hatua pia zinapigwa kukabili mabadiliko ya tabianchi-Guterres

Kuna changamoto lakini hatua pia zinapigwa kukabili mabadiliko ya tabianchi-Guterres

Mabadiliko ya tabianchi ni makubwa na tishio kwa amani, ustawi na malengo yote ya maendeleo endelevu na kwamba kukabili mabadiliko hayo ni fursa ambayo dunia haitomudu kuikataa.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres katika mjadala wa ngazi ya juu Alhamisi kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa ukijikita katika mabadiliko ya tabianchi na ajenda ya maendeleo endelevu SDG’s.

Guteres ameongeza kuwa hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi ni lazima, na hakuna mjadala kwamba zinahitajika kuchukuliwa haraka na bila upinzani

(SAUTI YA GUTERRES )

“Tunakabiliana na ukweli wa kisayansi na sio siasa, na ukweli uko bayana mabadiliko ya tabia nchi pekee ni tishio na linaleta vitisho vingine vingi. Tunakabiliwa na hatari kubwa katika ajenda nzima ya 2030”

Amesema licha ya changamoto zilizopo kuna matumaini

(SAUTI YA GUTERRES )

“Kuna ushahidi kwamba hata kama kuna baadhi ya serikali za kitaifa zimekengeuka katika ahadi, juhudi za pamoja za serikali za wilaya na taifa, biashara na asasi za kiraia, zimeunda kasi isiyositishwa”.