Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwezesha vijana katika afya ya uzazi-UNFPA Tanzania

Kuwezesha vijana katika afya ya uzazi-UNFPA Tanzania

Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA nchini Tanzania, limezindua mradi maalum wa mafunzo kwa ajili ya kuwawezesha vijana katika kuibua suluhu bunifu zinazohusu masuala ya afya ya uzazi.

Mradi huo wa miezi sita uitwao Amua, unatarajia kutumia teknolojia ya habari na mawasiliao TEHAMA na utawawezesha vijana wajasiriamali, kwa kuwapa mafunzo ya ujuzi kama sehemu ya kichocheo katika kukabiliana na changamoto za afya ya uzazi ambapo mawazo bora yataendelezwa kwa kupatiwa fedha za mitaji.

Robert Ngalomba ni Mtalamu wa teknolojia ya habari na mawasiliano ( ICT) wa UNFPA Tanzania.

( Sauti Ngalomba)