Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

SheTrades yafungua milango Rwanda, wanawake wazungumza

SheTrades yafungua milango Rwanda, wanawake wazungumza

Mpango wa SheTrades wa kuwezesha wanawake kupenya katika masoko ya kikanda na kimataifa umefungua milango yake huko Rwanda ambapo Mkurungezi Mtendaji wa kituo cha biashara cha kimataifa, ITC, Arancha Gonzales amesema ni fursa mpya ya kuimarisha harakati za nchi hiyo kumkomboa mwanamke.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo mjini Kigali, Bi. Gonzales amesema ni kwa mantiki hiyo anapongeza kampuni ya mtandao wa simu, MTN ambayo

(Sauti ya Arancha)

“Itasaidia kuunganisha wanawake na masoko, tumeahidiwa na shirika la kiraia la New Faces New Voices ambalo litaungnisha wanawake 3000 nchini Rwanda na masoko ifikapo mwaka 2020. Tumesikia ahadi kutoka serikalini kuwa watapunguza pengo la teknolojia.”

Mgeni rasmi alikuwa Jeannette Kagame, mke wa Rais wa Rwanda ambaye amesema SheTrade Rwanda..

(Sauti ya Jeannette)

“Matumaini yetu ni kwamba uzinduzi wa SheTrades nchini Rwanda itahamasisha wanawake wengi na mpango huu ili nao pia wanaweza kupata taarifa na fursa ambazo sasa zinanufaisha wanawake wachache wa Rwanda.”

Naye Linda Mukangonga, afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Haute Baso inayotengeneza mikufu na hereni kutokana na lulu amesema wamerahisishiwa kupata soko na pia kuleta pamoja wajasiriamali wanawake na kwamba..

(Sauti ya Linda)

“Inaweka mazingira ya ushirikiano kwani kuna wanawake wengi wenye mawazo thabiti na bora kuhusu biashara, kwa hiyo kwa kutuweka sote pamoja ni jambo zuri sana kwangu. Nadhani ina fursa nzuri ya biashara kwenye sekta yetu.”

ITC ni taasisi tangu ya kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD na mpango wake wa SheTrades uliozinduliwa mwaka 2015, unalenga kuunganisha wanawake milioni moja duniani kote ifikapo mwaka 2