Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuelekea uchaguzi mkuu Kenya, wanawake wajengewa uwezo wa mawasiliano

Kuelekea uchaguzi mkuu Kenya, wanawake wajengewa uwezo wa mawasiliano

Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Kenya mwezi Agosti mwaka huu, serikali imechukua hatua kujengea uwezo wanawake wanaowania nafasi mbali mbali za uongozi ili kufanikisha usawa wa 50 kwa 50 kwenye ngazi ya uamuzi ifikapo mwaka 2030.

Akihojiwa na Idhaa hii kando ya mkutano wa 61 wa kamisheni ya hadhi ya wanawake duniani, CSW61 jijini New York, Marekani, Waziri wa umma, vijana na jinsia Sicily Kariuki ametaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kuwapatia wagombea wanawake vikasha maalum vyenye maelekezo na mbinu..

(Sauti ya Sicily)

Kama hiyo  haitoshi, wanashirikiana pia na vyombo vya habari kutangaza na kuchapisha wasifu wa wanawake viongozi wa sasa ili.

(Sauti ya Sicily)