Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majitaka yaweza kuwa raslimali muhimu kwa kilimo-FAO

Majitaka yaweza kuwa raslimali muhimu kwa kilimo-FAO

Maji ni raslimali muhimu sana katika kufanikisha ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, limesema shirika la chakula na kilimo FAO. Katika kuadhimisha siku ya maji duniani ambapo kauli mbiu mwaka huu ni “majitaka” upunguzaji na utumiaji tena wa maji hayo,  FAO imesema  kimataifa zaidi ya asilimia 80 ya maji taka yanayozalishwa na jamii hurejea tena katika mfumo bila kutiwa dawa, kusafishwa au kutumika tena. Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Limeongeza kuwa endapo maji taka hayo yangetiwa dawa na kutuimika ipasavyo, ni rasilimali yenye thamani kwa upatikanaji wa huduma ya maji na lishe, kuchangia katika uhakika wa chakula na kuboresha maisha ya watu

Kukiwa na ongezeko kubwa la mahitaji ya bidhaa za kilimo, wakulima wanatafuta njia mbadala ya vyanzo vya maji . Na maji taka ya majumbani na mifumo ya umma ni kivutio kwao hususani katika maeneo ambayo huduma ya maji ya kawaida ni haba.

Kwa mantiki hiyo FAO inasema maji taka yaonekane kama rasilimali na sio mzigo wa kutupwa. Ndio maana shirika hilo na mengine yanayohusika na maji yanachagiza matumizi salama ya maji taka hususani kwenye kilimo.