Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushairi unatupatia matumaini katika wakati huu mgumu-UNESCO

Ushairi unatupatia matumaini katika wakati huu mgumu-UNESCO

Ushairi unatupa matumaini limesema shirika la Umoja wa mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO, katika kuadhimisha siku ya ushairi duniani , likipongeza uwezo wa aya kutupumzisha na misukosuko ya maisha ya kila siku na kutukumbusha uzuri wa wale wanaotuzunguka na muhimili utu wa pamoja.

Katika ujumbe maalumu wa siku hii mkurugenzi mkuu wa UNESCO Irina Bokova akinukuu utenzi wa mshairi Henry Wadsworth Longfellow amesema

Hatuna mabawa , hatuwezi kuruka

Lakini tuna miguu ya kutembea na kukwea

Kwa mwendo wa polepole , zaidi na zaidi

Hadi kilele cha mawingu ya wakati wetu

Ameongeza kuwa kama ilivyo ya kale lugha yake , ushairi unasalia kuwa muhimu zaidi sasa kuliko wakati mwingine wowote , katika wakati wa misukosuko kama chanzo cha matumaini, na kama njia ya kushirikiana nini maana ya kuishi katika dunia hii.

UNESCO iliitangaza tarehe 21 Machi kuwa siku ya ushairi duniani mwaka 1999 , ikiuita ushairi kamhitaji la kijamii ambalo huwakumbusha watu walikotoka.