Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatiwa hofu na kurejeshwa kwa wakimbizi wa Nigeria kutoka Cameroon

UNHCR yatiwa hofu na kurejeshwa kwa wakimbizi wa Nigeria kutoka Cameroon

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limesema linatiwa hofu na kuendelea kulazimishwa kwa mamia ya wakimbizi wa Nigeria walioko Cameroon kurejea nyumbani Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, licha ya kutiwa saini hivi karibuni kwa makubaliano ya pande tatu ambayo pamoja na mambo mengine yana lengo la kuhakikisha wakimbizi wanarejea kwa hiyari.

Shirika hilo linasema hadi sasa Cameroon imewawarudisha kwa nguvu kwenye vijiji vya mpaka wa Nigeria wakimbizi 2600.

Hofu ya UNHCR ni kwamba shuruti hii inafanyika baada ya kutia saini mufaka wa wakimbizi kurejea kwa hiyari na wakati ambapo hali ya usalama itaruhusu. Babar Baloch ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA BABAR BALOCH)

"Familia zimesambaratishwa na watoto wakatenganishwa na wazazi wao na wengi kuachwa nyuma. Wakimbizi ambao tayari wamerudishwa wanapewa msaada wa kibinadamu  ikiwemo maji na chakula na mashirika sita na kwa sasa wanaishi katika kambi la wakimbizi wa ndani ya Banki ."