Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maisha ya watu chupuchupu kwenye ajali ya ndege Wau-UNMISS

Maisha ya watu chupuchupu kwenye ajali ya ndege Wau-UNMISS

Mpango wa Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini UNMIS leo Jumatatu umesaidia kunusuru maisha ya watu baada ya ndege iliyokuwa na abiria 43 kuanguka  kwenye uwanja wa ndege wa Wau na kulipuka.

Ofisi ya UNMISS Wau ilikimbiza timu ya dharura kusaidia operesheni za ukozi, ikwa na madaktari, na askari wa zimamoto. Waloshuhudia wamesema ndege hiyo ya shirika la ndege la South Supreme ilikuwa ikijaribu kutua , iliposerereka nje ya mkondo na kushika moto.

Gavana wa Wau Andrea Mayar Anchor amewaambia waandishi wa habari kwenye eneo la tukio kwamba ukungu mkubwa umechangia ajali hiyo ambapo ndege ilishika moto ilipojaribu kutua

SAUTI ANHOR)

“Kulikuwa na ukungu na kuona ilikuwa shida . hivyo rubani alikaribia uwanja wa ndege kutokea upande wa  mto Jur na kuhamia kushoto  ili kutua. Wakati akitua akagonga gari la zimamoto.”

Ameongeza kuwa kwa bahati abiria wengi wamenusurika

(ANCHOR CUT 2)

“Kesho Inshallah tutakuwa na taarifa zote, Hizi ni taarifa chache nilizonazo sasa, lakini abiria wengi wamenusurika.