Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati yahaki za watu wenye ulemavu kuwa na mwanamke mmoja tu si sahihi

Kamati yahaki za watu wenye ulemavu kuwa na mwanamke mmoja tu si sahihi

Ukweli kwamba kuna mwanamke mmoja tu aliyechaguliwa na nchi wanachama kufanya kazi kwenye kamati ya haki za watu wenye ulemavu kimsingi sio sawa.

Huo ni ujumbe bayana uliowasilishwa na naibu kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Kate Gilmore katika ufunguzi wa kikao cha 17 cha kamati hiyo mjini Geneva, Uswisi.

Amezungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliyeliweka suala la usawa wa kijinsia katika uwakilishi wa wanawake kama kitovu cha uongozi wake .

Bi Gilmore amesema wakati nchi wanachama wanawajibika kwa kutokuweopo uwakilishi unaostahili kwenye kamati, kuna mengi bado yanaweza kufanyika.

“Tunawataka muhakikishe kuna msingi imara katika ajenda yenu mwaka huu , na tunawataka mchukue hatua maalumu kuhakikisha kwamba sauti na uzoefu wa wasichana na wanawake zinapatiwa nafasi katika maamuzi yenu.”

Amewataka nchi wanachama kurekebisha hali hii isiyokubalika katika uchaguzi ujao kwenye kamati hiyo ya haki za watu wenye ulemavu, kikao cha sasa kitakwisha April 12.