Skip to main content

Smurfs waing’arisha siku ya furaha

Smurfs waing’arisha siku ya furaha

Leo ni siku ya kimataifa ya furaha, siku ambayo hutumiwa na jumuiya ya kimataifa katika kuchochea amani na utengamano miongoni mwa jamii ili kukuza maendeleo. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Nats!

Hao ni vikaragosi wa filamu ya Smurfs wakipatiana ushauri kuwa wasile mgao wote wa chakula, kwani ni lazima kuwa makini katika matumizi endelevu ya rasilimali ili kila mmoja apate na hatimaye awe na furaha.

Vikaragosi hao wanatumiwa na Umoja wa Mataifa katika hamasa ya umuhimu wa kuishi pamoja kwa amani na furaha.

Hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, kumekuwa na tukio maalum la kuienzi siku hiyo, mkutano ukiangazia sera za umma kuhusu furaha.

Akizungumza katika mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J Mohammed amesema umoja huo unatizama furaha kama haki na kwamba licha ya tafsri tofauti za furaha lakini...

(Sauti Amina)

‘Sote kati yetu tunakubaliana kwamba maana muhimu inapatikana katika utangulizi wa katiba ya Umoja wa Mataifa, ambapo nchi zimeahidi kukuza kiwango bora cha maisha na uhuru mkuu. Maisha bora na uhuru kwa ajili yetu na familia zetu, jamii zetu  na nchi zetu. Nadhani hicho ndicho tunachokihitaji sote.’’

Kwa mujibu wa ripoti ya viwango mbalimbali vya furaha katika nchi mbalimbali iliyochapishwa katika wavuti maalum unaoangazia siku hiyo, nchi ya kwanza kwa furaha duniani ni Norway, bara la Afrika limetajwa kuwa nchi nyingi hazina furaha huku kiwango cha furaha kwa bara la Amerika kikiripotiwa kuporomoka.

Wakizungumzia umuhimu wa furaha katika maisha, wakazi nchini Uganda wanataja kile ambacho huwapa furaha.

(Sauti waganda)