Kenya yakabiliana na saratani

20 Machi 2017

[caption id="attachment_308680" align="aligncenter" width="620"]dailynews057d-17

Mkutano wa 61 wa hadhi ya wanawake CSW61 ukiendelea mjini New York Marekani, mke wa Gavana wa kaunti ya Meru nchini Kenya Phoebe Munya amesema ukosefu wa madaktari wa saratani umekuwa changamoto hususani kwa wanawake jambo lililosababisha kuchukua hatua kunusuru wanawake.

Katika mahojiano na idhaa hii Bi Munya amesema afya ya uzazi kwa wanawake ni kipaumbele chake na katika uwakilishi wake katika mkutano huo na anataja hatua zinachokuliwa ili kutoa usaidizi kwa wanawake.

(Sauti Bi Munya)

Amesema mwamko wa akina mama ambao haukutarajiwa awali unahamasisha kuendeleza juhudi za kukabiliana na saratani hususani ya shingo ya kizazi inayowashambulia wanawake.