Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utawala bora Tanzania umechochea ufadhili wetu- Benki ya Dunia

Utawala bora Tanzania umechochea ufadhili wetu- Benki ya Dunia

Nchini Tanzania hii leo, Rais wa Benki ya dunia Jim Yong Kim na Rais John Magufuli wameweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za juu katika eneo la Ubungo kwenye mkoa wa Dar es salaam, moja ya miradi inayofadhiliwa na benki hiyo.

Wakati wa kuelekea katika tukio hilo, Rais Magufuli na mgeni wake walisafiri kwa kutumia basi liendalo haraka, ambalo pia ni moja ya miradi inayofadhiliwa na benki hiyo kuboresha usafiri jijini Dar es salaam.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Rais Magufuli ametoa hakikisho..

(Sauti ya Magufuli)

Naye Dkt. Jim amesifu Tanzania kwa utawala bora wakati huu ambapo usimamizi bora wa fedha za miradi ni muhimu ili kulinda imani ya wahisani..

(sauti ya Dkt. Jim)

“Kile tulichojifunza kote duniani ni kwamba utawala thabiti kama mlionao hapa Tanzania ni muhimu kwasababu ufadhili wowote wa maendeleo kwa siku za usoni utapaswa kuwa ubia wa rasilimali za umma na zile za binafsi."