Skip to main content

ILO na wakfu wa Walk Free kuvalia njuga utumwa wa kisasa

ILO na wakfu wa Walk Free kuvalia njuga utumwa wa kisasa

Shirika la kazi duniani ILO na wakfu wa walk Free watashirikiana kutafiti kiwango cha utumwa wa kisasa duniani .Katika ushirika huo uliotangazwa mwishoni mwa wiki, mashirika hayo mawili yataanzisha makadirio ya pamoja ya utumwa wa kisasa kwa nia ya mchakato wa kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs, huku yakijiwekea kiwango cha asilimia 8.7.

Makadirio hayo ya kimataifa yatakayotokana na mahojiano mbalimbali ya ana kwa ana, yatatoa mwangaza zaidi ya idadi ya walio katika utumwa huo wa kisasa, katika kanda, umri na jinsia.

Pia watalishirikisha shirika la kimataifa la uhamiaji IOM ambalo litasaidia kutoa msaada wa utafiti hasa kwa mgogoro wa wahamiaji.