Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunahitaji fedha za dharura kusaidia wakimbizi wa Iraq: UNHCR

Tunahitaji fedha za dharura kusaidia wakimbizi wa Iraq: UNHCR

Idadi ya wanaofurushwa makwao ikiongezeka Magharibi mwa Mosul nchini Iraq, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linafungua kambi mpya sambamba na wito wa usaidizi kwa wafadhili kuongeza fedha kwa ajili ya ulinzi na malazi kwa wanaofurushwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya UNHCR, watu 255,000 wamefurushwa kutoka Mosul na maeneo ya karibu tangu mwezi Oktoba mwaka jana, ikiwa ni pamoja na zaidi ya 100,000 tangu kampeni ya kijeshi iliponza Magharibi mwa mji huo mnamo Januari 19.

UNHCR inasema juma lililopita limeshudia kiwango cha juu cha watu waliofurushwa ambapo watu 32,000 wamekimbia makwao tangu Machi 12 hadi 15.

Kiasi cha dola milioni 212 kinahitajika kwa mwaka huu wa 2017 , kiasi kidogo kati ya hicho kikiwa kimetolewa, ambapo shirika hilo la kuhudumia wakimbizi limesema linahitaji msaada wadharura ilii kuwasaidia wakimbizi wa ndani wanaovuka kutoka Iraq kuelekea Syria.

UNHCR imesema ombi la msaada huo pia linahusisha dola milioni saba zinazohitajika katika siku 10 zijazo na dola milioni 30 zinazohitajika katika majuma mawili yajayo.