IOM yakaribisha hatua kubwa ya kuwahamiasha waomba hifadhi 10,000 kutoka Ugiriki

17 Machi 2017

Zaidi ya waomba hifadhi 10,000 sasa wamehamishwa kutoka Ugiriki na kwenda kwenye mataifa menmgine ya Muungano wa Ulaya . Grace Kaneiya na taarifa kamili

(TAARIFA YA GRACE)

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM waomba hifadhi hao wamehamishwa chini ya utekelezaji wa mpango wa Muungano wa Ulaya ulioanza mwanzoni mwa Machi wa kuwahamisha maelfu ya watu hao kutoka Ugiriki.

Tangu ulipoanza watu 367 wameshapelekwa Ubelgiji, Estonia, Ujerumani,, Malta, Ureneo, Slovenia na Hispania na kufikisha idadi ya watu ambao tayari wameshahamishwa kutoka Ugiriki kufikia 10,004.

Watu wengine 475 walihamishwa kutoka Italia katika kipindi hichohicho. Na IOM inasema ni hatua nzuri ya kuwapa makazi waomba hifadhi, ikiongeza kuwa jumla ya watu wote waliokwishahamishwa kutoka Ugiriki na Italia tangu operesheni ilipozinduliwa rasmi mwezi Oktoba 2015 ni zaidi ya elfu kumi na nne.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter