Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka mmoja baada ya kufungwa mpaka wa Balkan watoto wazidi kua hatarini:UNICEF

Mwaka mmoja baada ya kufungwa mpaka wa Balkan watoto wazidi kua hatarini:UNICEF

Mwaka mmoja baada ya mpaka wa mataifa ya Balkan kufungwa na Muungano wa Ulaya na serikali ya Uturuki kutoa tamko lenye lengo la kuzuia wimbi la wahamiaji, watoto wakimbizi na wahamiaji wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi ya kurejeshwa kwa nguvu, kuwekwa rumande, kunyanyaswa na kunyimwa haki.

Hayo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNICEF, likiongeza kwamba ingawa kumekuwa na kupungua kwa idadi ya watoto wanaoingia Ulaya tangu Machi mwaka jana, kumekuwa na ongezeko la vitisho na madhila kwa watoto wakimbizi na wahamiaji, kwani umekuwa ni mzunguko wa mateso, watoto wanakimbia machafufuko na wanaishia kukimbia tena, kukabiliana na jela au hata kutelekezwa.