Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usugu wa viuavijasumu ni tisho kwa kwa maendeleo endelevu: UM

Usugu wa viuavijasumu ni tisho kwa kwa maendeleo endelevu: UM

Usugu wa viuavijasumu au antimicrobial resistance AMR ni tisho kubwa la kutimiza ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu amesema naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed.

Amesema hayo hivi leo Alhamisi kwenye makau makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York walipokuwa wakijadili swala hilo na mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO Dkt. Margaret Chan.

Bi Mohamed amesema dhamira ya kuundwa kwa kundi maalum la kushughulia na tatizo ni hilo kwa ngazi za juu ni kupambana AMR, na kushauriana kuhusu jitihada za kimataifa jinsi wanavyokabiliana na tisho hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari amesema kwamba AMR inaathiri binadamu na afya ya wanyama, kilimo, mazingira ya kimataifa na biashara na kwamba...

(Sauti ya Mohamed)  

"Tukiwa tunaingia kwenye mfumo wa maendeleo endelevu ningependa kusisitiza kwamba AMR kwa kweli ni tisho ili kufikia SDGs, hasa katika nchi zetu zinazoendelea. AMR ina madhara makubwa dhidi  ya uwezo wetu kuhakikisha maji safi, uzalishaji wa chakula endelevu na kuondoa umaskini”.

Naye Dkt Margaret Chan ambaye ni mwenyekiti mwenza wa kundi maalum hilo amesema tayari wanashirikiana na mashirika mengine ikiwemo FAO na serikali kukabaliana na tatizo hili.

Ameongeza ufumbuzi wa uratibu huu ni hatua iliyokubaliwa wakati wa mkutano wa ngazi ya juu wa baraza kuu mwaka jana hapa kwenye makao makuu.

Akitoa shukrani zako kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti mwenza na Bi Mohamed amesema kuwa...

(Sauti ya Dkt Chan)

"Tumefurahi sana na mtaona orodha ya wataalam kutoka nchi tofauti na kutoka kwa mashirika mbali mbali ambao tutafanya kazi pamoja kufuata uongozi wa serikali tofauti za dunia, kama mnavyokumbuka mwongozo huo ulipitishwa kwenye kikao cha Umoja wa Mataifa mwaka jana."