Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya raia 120,000 wamekimbia madhila magharibi mwa Mosul, Iraq

Zaidi ya raia 120,000 wamekimbia madhila magharibi mwa Mosul, Iraq

Tangu vikosi vya kijeshi nchini vianze mapigano ya kukomboa mji wa Mosul mwezi Oktoba mwaka, takribani raia 345,000 wamekimbia makwao, ambapo 275,000 kati yao wanahitaji usaidizi.

Amesema mratibu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Bi Lise Grande akizungumza na waandishi wa habari hii leo kwa njia ya video kutoka Iraq.

Ameongeza inakadiriwa kuna raia zaidi ya Laki Nane magharibi mwa Mosul ambako mapigano ya kukomboa yalianza mwezi Februari na tayari zaidi ya 120,000 wamekimbia makazi yao..

(Sauti ya Lise Grande)

“Hao 120,000 wanaokimbia wako katika hali mbaya, familia nyingi tulizohoji wanasema hawana chakula cha kutosha na wanalazimika kupata mlo mmoja kwa siku, au kwa siku kadhaa kwa sababu hawana fedha za kuweza hata kununua chakula na pia wana uhaba mkubwa wa maji."

Amesema ijapokuwa jukumu hilo ni la serikali, wanaposaidia wanakuta kwamba..

(Sauti ya Lise Grande) 

"Kwa vile wanaokimbia wanatoka kwa kasi inatubidi kuharakisha misaada ikiwemo ujenzi ambapo kati ya maeneo yote haya ya kusini, magharibi na mashariki mwa Mosul tumeanzisha vituo 17 vya dharura vya misaada ambavyo vinawapokea. Namna inavyofanya kazi ni kwamba tunafanya ujenzi kwa saa ishirini na nne. Maeneo yanapatikana na ujenzi wa mahema, upelekaji wa magodoro na vifaa vya kujisafi tunafahimisha majeshi. "