Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili na manyanyaso kazini ni ukiukaji wa haki za binadamu: ILO

Ukatili na manyanyaso kazini ni ukiukaji wa haki za binadamu: ILO

Ukatili na manyanyaso kazini dhidi ya wanawake ni tatizo kubwa na la kimataifa limesema shirika la kazi duniani ILO.

Akizungumza kwenye mjadala maalumu kandoni mwa kikao cha 61 cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani uliojadidili ukomeshaji wa ukatili wa wanawake kazini, , Manuela Tomei ambaye ni mkurugenzi wa idara ya hali ya kazi na usawa kwenye shirika la ILO amesema vitendo hivyo ni ukiukwaji wa haki za binadamu na vinaathiri utendaji wa kazi sio tu kwa waathirika, bali kwa viongozi na kampuni au mashirika wanayofanyia kazi , kwa hiyo ni lazima vikomeshwe

(SAUTI YA MANUELA TOMEI)

“Hili ni tatizo la kimataifa na linaathiri wanawake wote , bila kujali kiwango chao cha elimu na wapi wanakofanya kazi . Huu ni ukiukaji wa haki za binadamu , ni tishio kwa utu wa mwanamke, kwa usalama wa mwanmke ukiwemo wa kipato, kwa afya yao na maisha yao. Kazi zenye hadhi ni muhimu kwa uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake kwa hivyo ukatili katika ulimwengu wa kazi ni tisho kwa uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.”