Ukwepaji sheria ndio adha kubwa Sudan kusini-UM

Ukwepaji sheria ndio adha kubwa Sudan kusini-UM

Tume ya Umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu Sudan Kusini, imesema hali ya kibinadamu inaendelea kuzorota nchini humo, huku uvunjaji wa sheria, watu kuswekwa rumande kiholela, utesaji, ubakaji na mauaji vikigeuka kuwa kasumba. Taarifa kamili na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Mwenyekiti wa tume hiyo Yasmin Sooka ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutia msukumo wa kuanzishwa mahakama ya mseto kama moja ya mapendekezo ya kuimarisha hali ya haki za binadamu nchini humo. Akihojiwa na Radio Miraya ya Umoja wa Mataifa Bi Sooka amesema shida kubwa Sudan Kusini ni watu kutowajibishwa.

(Sauti ya Sooka)

“Moja ya matatizo Sudan Kusini ni ukwepaji wa sheria na hivyo huwezi kudai kuwa unataka amani kwanza bila kuwepo na haki. Amani na haki ni vitu viwili vilivyo upande mmoja wa shilingi na vinakwenda sanjari, na bila haki huwezi kuwa na amani endelevu.”