Skip to main content

Wahisani endelezeni usaidizi kwa CAR, hali inadorora

Wahisani endelezeni usaidizi kwa CAR, hali inadorora

Hali ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR inazidi kudorora tangu kuanza upya kwa mapigano mwezi Septemba mwaka jana hadi mwezi huu wa Machi. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA)

Kaimu mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Michel Yao amesema hayo wakati wa kikao cha wahisani wa CAR kilichofanyika Yaounde, Cameroon.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Waziri wa masuala ya kibinadamu wa CAR ambapo kwa pamoja walieleza kuwa ghasia zimeibua zaidi ya wakimbizi wapya wa ndani 100,000 na hivyo idadi ya wakimbizi wa ndani sasa ni zaidi ya laki nne.

Bwana Yao amesema idadi hiyo imeibua pia mahitaji mapya ya kibinadamu ilhali ni asilimia tano tu ya ombi la dola takribani milioni 400 ndio zimepatikana.

Wamesema ufadhili ukizidi kupungua hata mafanikio yaliyopatikana katika kuboresha sekta za kijamii kama vile elimu na afya yatatokomea hivyo wametoa wito kwa wahisani kuendeleza ukarimu wao kwa CAR.