Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lajadili jinsi ya kukomesha usafirishaji haramu wa binadamu

Baraza la usalama lajadili jinsi ya kukomesha usafirishaji haramu wa binadamu

barazauhalifu

Takwimu bora na ufadhili vitakuwa muhimu sana katika vita vya kimataifa vya kukomesha biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres Jumatano akihutubia baraza la usalama.

Mabalozi kutoka nchi wanachama wamekutana kujadili njia za kuzuia mitandao ambayo inafaidika na uhalifu kama kazi za shutruti, uhalifu ambao Umoja wa Mataifa unasema unaingiza dola bilioni  150 kila mwaka.

Guterres amesema utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu ya

mwaka 2030 utaweza kusaidia kuvunja minyororo ya uhalifu huo

(GUTERRES CUT)

“Malengo matatu yanashughulikia usafirishaji haramu wa binadamu, ikiwemo usafirishaki haramu kwa ajili ya biashara ya ngono, kazi za shuruti, ajira kwa watoto na uingizaji na utumiaji wa watoto jeshini. Takwimu bora itakuwa na ufadhili itakuwa muhimu sana . Umoja wa Mataifa umejidhatiti sio tu kuwasaidia wahanga bali kujumuisha sauti zao , wakati tukiandaa na kutekeleza mikakati ya kukomesha usafirishaji haramu.”

Naye mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na dawa na uhalifu UNODC Bwana Yury Fedotov amesema wahalifu hutumia fursa ya adha yaw engine kujinufaisha

(SAUTI FEDOTOV)

"Wakati vita vikisambaratisha watu na utawala wa sheria ukivunjika , wahalifu wanapata mwanya wa biashara kupitia mitandao ya uhalifu wa kupangwa wa usafirishaji haramu wa watu duniani. Jambo ambalo linaimarika zaidi na visa vidogo vya uwajibishaji vinavyoripotiwa kote duniani. "