Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maarifa ni sehemu kubwa ya ukuaji wa uchumi duniani-WIPO

Maarifa ni sehemu kubwa ya ukuaji wa uchumi duniani-WIPO

Shughuli za uchumi kote duniani zina kipengee muhimu cha maarifa kuliko wakati mwingine wowote, kwa mujibu wa takwimu za karibuni zilizotolewa na shirika la kimataifa la hati miliki (WIPO).

Katika Ripoti yake kwa mwaka 2016 shirika hilo linasema limeshuhudia idadi kubwa ya maombi ya kimataifa ya kulinda masuala ya ubunifu, nembo za biashara na mitindo ya viwandani. Miongoni mwa nchi zilizotuma maombi mengi ni Japan, Uchina, Ujerumani na Jamhuri ya watu wa Korea. WIPO ni jukwaa la kimataifa kwa ajili ya huduma za hati miliki, sera , taarifa na ushirikiano.

Uchina kiwango chake cha maombi kimeongezeka kwa asilimia 44.7 na kama mwenendo huo utaendelea basi WIPO inasema itaipita Marekani ambaye ni mtumiaji mkubwa wa mkataba wa ushirikiano wa masuala ya hati miliki katika miaka miwili ijayo.

Mkurugenzi mkuu wa WIPO ni Francis Gurry.

(SAUTI YA GURRY)

"Kiwango cha ongezeko la maombi ya kimataifa ya kulinda ubunifu ni asilimia 7.3. Ukuaji wa kimataifa wa maombi ya nembo ni asilimia 7.2 na kwa mitindo ni asilimia 35. Kinachosemekana ni kwamba  shughuli nyingi za kiuchumi zina kipengee muhimu cha maarifa zaidi na zaidi na kwamba sekta hizi za uchumi zina kasumba ya kufanya vyema kuliko sekta zingine za uchumi”