Skip to main content

Wanawake wakishiriki katika uongozi huchochea maendeleo

Wanawake wakishiriki katika uongozi huchochea maendeleo

Mkutano 61 wa kamisheni ya hadhi ya wanawake duniani CSW, unaendelea  kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, leo pamoja na mambo mengine mjadala unajikita zaidi katika uwezeshaji wa wanawake na malengo ya maendeleo endelvu SDGs.

Wawakilishi wa makundi ya wanawake kutoka mashinani hususani barani Afrika wanaeleza changamoto na mafaniko katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

Miongoni mwao ni Priscilla Oparanya kutoka kaunti ya Kakamega nchini Kenya, ambaye ameiambia idhaa hii katika mahojiano maalum kuwa ushiriki wa wanawake katika uongozi ni muhimu katika maendeleo.

 (Sauti Priscilla)