Wakimbizi wanawake Kigoma wapewa misaada

Wakimbizi wanawake Kigoma wapewa misaada

Wanawake wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma Tanzania wamepatiwa misaada ya vifaa vya kujisafi ikiwa ni sahemu ya kuhifadhi hadhi za wanawake ambao hukabiliwa na changamoto nyingi hususani wawapo ukimbizini.

Katika mahojiano na Simavu Nangolo wa redio wa shirika Umoja Radio ya Nyarugusu Kigoma, Meneja wa shirika la Twesa Alex Ndondeye, shirika ambalo hufanya kazi kwa ubia na lile la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, ameeleza kundi lengwa kwa misaada hiyo ikiwamo taulo za kike, ndoo na sabuni.

(Sauti Alex)

Naye mmoja wa wanufaika wa msaada huo hakuficha hisia zake.

(Sauti Mnufaika)