Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan Kusini imeanza kuwahamisha watu kwa kuzingatia makabila yao

Sudan Kusini imeanza kuwahamisha watu kwa kuzingatia makabila yao

Serikali ya Sudan Kusini imeanza kampeni ya kuorodhesha na kuhamisha watu kwa mujibu wa makabila yao amesema mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.

Yasmin Sooka ambaye pia ni mwenyekiti wa tume maalumu ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi wa haki za binadamu Sudan Kusini, akizungumza kwenye baraza la haki za binadamu mjini Geneva amesema wakati vita vya wenyewe kwa wenye vikiendelea nchini humo , kitendo cha serikali kuchora upya mipaka kimepunguza idadi ya watu wa kabila la Shilluk na Nuer kwenye jimbo la Upper Nile .

(Sauti ya Yasmin)

"Ripoti yetu inaainisha kwamba raia wa sudan kusini wanalengwa kwa maksudi kwa  misingi ya kabila na serikali na vikosi vinavyounga serikali, wanauwawa, kuwatekwa nyara, kushikiliwa kiholela, kunyimwa uhuru wao, kubakwa na ukatili wa kingono, kuteketezwa kwa vijiji na kuporwa."