Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu wanahitaji msaada haraka baada ya kimbunga kuipiga Madagascar:IFRC

Maelfu wanahitaji msaada haraka baada ya kimbunga kuipiga Madagascar:IFRC

[caption id="attachment_312313" align="aligncenter" width="625"]madagascarkimbunga

Maelfu ya watu nchini Madagascar wanahitaji haraka misaada ya kibinadamu baada ya Kimbunga Enawo kupiga kisiwa hicho na kuharibu nyumba huku mafuriko ykiathiri mashamba na jamii ambapo shikisho la chama cha msalaba mwekundu IFRC limeanza kutoa msaada wa dharura.

Inakadiriwa kuwa watu kadhaa wamefariki dunia, karibu watu 200 kujeruhiwa na wengine zaidi ya 84,500 kuyahama makazi yao . Watu wengine karibu 300,000 katika wilaya 58 zilioathirika na dhoruba hilo pia wamekimbia makwaotangu Machi 7.

Mkurugenzi wa IFRC kanda ya Afrika Dkt Fatoumata Nafo-Traoré amesema uharibifu mkubwa umefanyika hasa kaskazini mwa nchi hiyo na maelfu wanahitaji msaada wa haraka wa makazi, chakula, matibabu, maji safi na huduma nyingine muhimu.

Chama cha msalaba mwekundu cha Malagasy kimepeleka timu ya watu 24 ili kukabiliana na maafa hayo ikiwa ni pamoja na watu 890 wa kujitolea, ambao wengi wao walikuwa tayari kwenye maeneo hayo kutoa onyo na ujumbe kabla ya dhoruba. Kwa sasa wanaendelea kutoa huduma ya kwanza, ushauri wa matibabu na msaada wa kisaikolojia kwa familia katika vituo vya uokoaji.

IFRC imezindua fungu la dharura la Francs 895,000 za Uswisi ili kuwezesha chama cha kitaifa cha msalaba mwekundu kuwasaidia watu angalau 25,000 walioathirika na kimbunga.

Shirika hilo litasambaza msaada wa vifaa vya jikoni, vifaa vingine vya lazima na vifaa vya dharura kama malazi na zana za ujenzi ili kukarabati nyumba zao.