Skip to main content

Mkurugenzi mkuu wa IOM azuru kituo cha wahamiaji Niger:

Mkurugenzi mkuu wa IOM azuru kituo cha wahamiaji Niger:

Mwishoni mwa juma, Mkurugeni mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, William Lacy Swing ameanza ziara ya siku tatu nchini Niger ambako amekutana na viongozi wa kitaifa na kikanda , na pia kutembelea kituo cha muda cha wahamiaj kwenye mji mkuu wa taifa hilo Niamey.

Bwana Swingi amekwenda pia katika mji wa jangwani wa Agadez. Akiwa Niamey amefanya mazungumzo na Rais wa Niger Issoufou Mahamadou,  Waziri mkuu Brigi Rafini, Waziri wa mambo ya ndani Mohamed Bazoum, Waziri wa mambo ya ndani wa Hispania Juan Ignacio Zoido Álvarez  na Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Bruno Le Roux.

Amekuwa na mawasiliano na timu ya Umoja wa Mataifa nchini Niger, ujumbe wa Muungano wa Ulaya na malozi wa nchi za Muungano wa Ulaya.

Na katika jimbo la Agadez alikoambatana na mabalozi wa Muungano wa Ulaya, Mali, Senegal na Marekani amekutana na meya wa jimbo hilo Rhissa Feltou.