Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Syria, janga kubwa zaidi la kibinadamu tangu vita ya kuu ya pili ya dunia: Zeid

Syria, janga kubwa zaidi la kibinadamu tangu vita ya kuu ya pili ya dunia: Zeid

Akilihutubia  jopo la ngazi ya juu la baraza la haki za binadamu mjini Geneva Uswisi hii leo,  Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa   Zeid Ra'ad Al Hussein, amesema vita vya Syria ni janga baya zaidi la kibinadamu tangu vita pili ya dunia. Taarifa kamili na Flora Nducha.

(Sauti ya Flora)

Zeid ambaye ametoa mfano wa namna janga hilo linavyoumiza maisha ya watu, amesema hivi kariuni amekutana na kundi la wanawake kutoka Syria  ambao ndugu zao wanashikiliwa vizuizini, au wametoweka kwa miaka mingi huku wao wenyewe wakiwa wahanga wa vitendo hivyo, na kuongeza kuwa idadi isiyohesabika ya watu wameteseka kwa kushikiliwa, kutekwa nyara na vitendo vingine nchini Syria.

Amesema madhila hayo yamelifanya taifa hilo kuwa ukanda wa mateso, hofu ya hali ya juu na ukiukwaji wa haki, na akasema licha ya juhudi za ombi la misaada  kwa ajili ya watu wa Allepo mwaka jana, inasikitisha kwamba ombi hilo halikuwagusa kabisa au kwa uchache viongozi wa dunia ambao ushawishi wao ungeweza kusaidia kukomesha vita vya Syria.