Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Buba waendelea kushambulia watoto duniani: WHO

Buba waendelea kushambulia watoto duniani: WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema ugonjwa wa buba ambao hushambulia zaidi watoto bado unazishambulia nchi 13 duniani, licha ya shirika hilo kutangaza mwaka jana kuwa  India haina tena ua.

Taarifa ya shirika hilo kuhusu ugonjwa huo inasema kuwa matibabu yake ni rahisi kwani dozi moja pekee ya kunywa ya dawa iitwayo kwa kitaalamu azithromycin, yatosha kuponya buba.

WHO imesema inawezekana kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo, ikiwa tu dawa hiyo inapatikana na hilo laweza kutekelezwa ifikapo mwaka 2020.

Buba ni moja ya magonjwa yatokanayo na bakteria sugu. Gonjwa hili linashombulia zaidi watoto lilikuwa miongoni mwa magonjwa yaliolengwa kutokomezwa na WHO na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, katika miaka ya 1950.