Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiukwaji wa haki za binadamu bado unaendelea Burundi:UM

Ukiukwaji wa haki za binadamu bado unaendelea Burundi:UM

Wajumbe wa tume maalumu ya wa tume ya uchunguzi kuhusu haki za binadamu nchini Burundi, Fatsah Ouguergouz, Reine Alapini Gansou na Françoise Hampson wamewasilisha ripoti yao ya kwanza kwa baraza la haki za binadamu wakisema wana wasiwasi kuhusu kiwango cha ukiukwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji mwingine kwa ujumla. Wasema kupitia mfululizo wa mahojiano yaliyofanywa na vyanzo mbalimbali imebainika kuwa mwenendo wa ukiukwaji ulioonekna 2015 na 2016 bado unaendelea. Akielezea baraza hilo mwenyekiti wa tume hiyo Fatsah Ouguergouz amesema...

(Sauti ya Fatsah) 

"Kwa mujibu wa taarifa kupitia mfululizo wa mahojiano, ukiukwaji wa haki ya kuishi na uadilifu uliendelea tangu 2015 katika njia ya usiri na kuchukua mifumo mipya. madai ya kutoweshwa kuongezeka, na watu kuwekwa kizuizini kusiko rasmi"

Tume hiyo iliyoanza kazi yake Novemba mwaka jana imebainisha kuendelea kwa visa vya kudai fidia kuongezeka kufuatia kudhoofika kwa utawala wa sheria nchini humo. Wajumbe hao wameelezea wasiwasi kuhusu kuitowajibishwa kwa waliohusika na ukatili huo kutoadhibiwa.

Wametoa wito kwa serikali ya Burundi kushirikiana na tume yao ikiwa ni pamoja na wanachama wa haki za binadamu, mataifa ya kikanda, Umoja wa Mataifa, Muungano wa Afrika na mashirika ya kikanda. Wametaja kuwa ushirikiano huo ni muhimu sana na kwamba watafanya uchunguzi wao kwa njia ya kitaalamu, huru na bila upendeleo na kusikiliza wadau wote. Tume hiyo itatoa ripoti yao nyingine kwa Baraza la Haki za Binadamu mwezi Juni na ripoti yao ya mwisho katika kikao 36 wa Baraza hilo mwezi Septemba.

Naye mwakilishi wa Burundi kwa Umoja wa Mataifa mjini Geneva Renovat Tabu akijibu shutma hizo amesema

(Sauti ya Tabu)

"Nchi yangu inataka pia kusikilizwa na jumuiya ya kimataifa, kuhukumiwa kwa haki, na kwamba juhudi zinazofanywa na Serikali ili kuboresha hali ya haki za binadamu kutambulika. Pia kuelewa kuwa ufumbuzi wa mgogoro ulioletwa na upinzani lazima kutatuliwa na waburundi wenyewe ndani ya taasisi za halali na uwezeshaji unaoendelea. Burundi ingependa kushirikiana na Baraza na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, lakini kwa heshima ya uhuru wake na sio inavyofanyika kwa muda fulani"