Skip to main content

Vijana wa kiume badilikeni, wajumuisheni wasichana-Kuria

Vijana wa kiume badilikeni, wajumuisheni wasichana-Kuria

Kelvin Macharia Kuria, Balozi wa vijana kutoka serikali ya Kenya, ni miongoni wa washiriki katika mkutano wa 61 wa kamisheni ya wanawake CSW, unaoendelea jijini New York, anasema mitizamo kwa vijana wa kiume kuhusu vijana wenzao wa kike ni nyenzo katika kuwawezesha wanawake kujumuishwa.

Kuria ameiambia idhaa hii katika mahojiano maalum kuwa nchini Kenya kuna mabadiliko makubwa ya kifikra katika kundi hilo lakini akasema bado kuna changamoto.

(Sauti Kuria)

Anasema kila ambacho anatamani kukiona kinatimia nchini humo.

(Sauti Kuria)