Skip to main content

Ukame umeyaweka rehani maisha ya watoto Somalia-UM

Ukame umeyaweka rehani maisha ya watoto Somalia-UM

Magonjwa yanayohusiana na ukame yamekatili maisha ya watoto 47 katika miiezi miwili iliyopita katika moja ya hospitali inayoendeshwa na serikali mjini Mohadishu Somalia. Rosemary Musumba na taarifa kamili

(TAARIFA YA ROSE)

Umoja wa Mataifa umetoa onyo kwa dunia kwamba athari za ukame ukichanganya na vita katika taiafa hilo la Pembe ya afrika zinaweza kuwa zahma kubwa, kwani takriban watu milioni tatu wako katika hatari ya baa la njaa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres hivi karibuni ametoa ombi la dola milioni 825 ili kuwasaidia watu zaidi ya milioni tano kwa miezio sita ijayo.

Kwa miezi miwili iliyopita Hospital Banaadir mjini Mogadishu, imetibu angalau watoto 1,200 wenye utapia mlo uliokithiri, na 47 kati yao kupoteza maisha. Dr Luul Mohamud Mohamed ni mkuu wa idara ya watoto hospitalini hapo

(SAUTI DR LUUL)

“Katika visavingi chanzo cha kifo ni ukosefu wa maji mwilini, tunajaribu kuwaongeza maji watoto na kuwapa vijiuavijasumu kwa sababu tunahisi wana hara kutokana na maji na kipindupindu. Haya ndio tunayofanya hadi sasa.”

Ukame mkali umewavungisha virago maelfu ya Wasomali kutoka katika nyumba na jamii zao.