Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biashara ya vyakula ofisini yaleta nuru kwa Nadine nchini Burundi

Biashara ya vyakula ofisini yaleta nuru kwa Nadine nchini Burundi

Malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs yanapigia chepuo harakati za wanawake kujikwamua iwe kiuchumi,kisiasa au kijamii. Matarajio ni kwamba kwa kufanya hivyo maisha ya mwanamke huyo na jamii yake yatakuwa bora na hatimaye ifikapo mwaka 2030 dunia itakuwa pahala salama na bora kwa kila mtu kuishi bila kujali jinsia yake. Nchini Burundi, Nadine Ishimwe baada ya kufiwa na mume wake aliona maisha yanaweza kwenda kombo kwa kuwa hakuwa na ajira. Hivyo alianzisha biashara ya kuuza vyaula kwenye ofisi jambo ambalo amesema limemletea nuru na amani kwake yeye na familia yake. Katika makala hii basi Ramadhani Kibuga mwandishi wetu wa maziwa makuu amepata fursa ya kuzungumza naye na anaanza kwa kuelezea ilikuwa vipi.