Badala ya kutuhurunmia tuwezesheni watu wenye ulemavu: Seneta Omondi

14 Machi 2017

Kikao cha 61 cha kamisheni ya hali ya wanawake kinaendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kikihusisha watu kutoka kila kundi kwenye jamii wakiwemo wenye ulemavu.

Wakipaza sauti zao wanasema kuwahurumia wanawake na wasichana wenye ulemavu hakuna tija, tuzingatie nmana ya kuwawezesha, hii ni kauli ya mmoja wa washiriki wa mkutano wa 61 kamisheni ya wanawake CSW, Seneta wa viti maalum kutoka Kenya Godliver Omondi.

Katika mahojino na idhaa hii kandoni mwa mkutano huo, Seneta Omondi ambaye ni mwanamke mwenye ulemavu akiwakilisha kundi hilo, amesema dhana ya kutumia muda mwingi kulihurumia kundi hilo haina nafasi, badala yake akashauri kufikiri namna ya kuwawezesha kulingana na mazingira yao. Akitoa mfano amesema.

(Sauti Omondi)

Bi Omondi ambaye anatarajia kushiriki katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mwaka huu kwa kushindana na watu wasio na ulemavu kunadi sera kwa wapiga kura, anasema katika mchakato wa uchaguzi changamoto ni.

(Sauti Omondi).

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter