Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka 2016 ulikithiri kwa ukatili dhidi ya watoto Syria-UNICEF

Mwaka 2016 ulikithiri kwa ukatili dhidi ya watoto Syria-UNICEF

Ikiwa inaelekea sasa mwaka wa saba tangukuzuka kwa mgogoro nchini Syria, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema kwa ukiukwaji dhidi ya watoto nchini humo ulikuwa mbaya zaidi 2016 ikilinganishwa na miaka mingine tangu vita kuanza. Rosemary Musumba na taarifa kamili.

( TAARIFA YA ROSE)

Nats!

Hao ni baadhi ya watoto wanokabiliwa na madhila mbalimbali nchini Syria, wakati huu ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema kwa ukiukwaji dhidi ya watoto nchini humo ulikuwa mbaya zaidi 2016 ikilinganishwa na miaka mingine tangu vita kuanza.

Mathalaani katika video hii yenye kutia simanzi watoto hawa wanatapatiwa tiba, afya zao zimezorota, na wanalia kwa uchungu.

UNICEF inasema kuwa habari za kuthibitishwa zinaeleza juu ya mauaji, ulemavu na ajira ya watoto iliyoongezeka kwa kasi mwaka jana katika hali ya vurugu kote nchini. Inakadiriwa kuwa watoto 652 waliuawa, ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 kutoka 2015 hadi 2016

Watoto 255 waliuawa katika au karibu na shule zao.

Taarifa hiyo pia imesema kuwa zaidi ya watoto 850 waliajiriwa kupigana katika vita, zaidi ya mara mbili ya idadi ya walioajiriwa 2015.