Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pazia la CSW 61, kamesheni ya hali ya wanawake lafunguliwa UM

Pazia la CSW 61, kamesheni ya hali ya wanawake lafunguliwa UM

Kikao cha 61 ya kamisheni ya hali ya wanawake duniani limefunguliwa hii leo kwenye makao makuu ya umoja wa Mataifa mjini New York. Amina Hassan na maelezo kamili

(TAARIFA YA AMINA)

Nats….

Mwenyekiti wa kikao hicho cha 61 chenye kauli mbiu “ wanawake katika ulimwengu wa kazi unaobadilika” akikaribisha wajumbe katika mkutano huo.

Wanawake kutoka katika kila pembe ya dunia na Nyanja mbalimbali wakiwemo wawakilishi wa serikali, asasi za kiraia , mashirika ya kimataifa, Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa masuala ya wanawake wanakutana kujadili na kutathimini hali ya wanawake na mustakhbali wao.

Baada ya ajenda ya mkutano kupitishwa ,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  António  Guterres akatoa ujumbe wake akipongeza hatua zilizopiogwa katika kuwawezesha wanawake lakini akasisitiza safari bado ndefu kwani..

image
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akihutubia CSW61.(Picha:UM/Rick Bajornas)
(SAUTI YA GUTERRES)

“Katika dunia ambayo inatawaliwa na mfumo dume, uwezeshaji wa wanawake ni lazima uwe kipaumbele. Wanawake tayari uwezo wa kufanikiwa, na uwezeshaji ni kutokomeza vikwazo kwa kimfumo. Wanaume bado wanatawala hata katika nchi ambazo zinachukuliwa zimepiga hatua. Mfumo dume unawakandamiza wanawake na hilo linamuaathiri kila mtu”

Naye mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake Phumzile Mlambo Ngcuka akafunguka kuwa wanawake wengi wanafanya kazi katika sekta isiyo rasmi na ujira ni mdogo au hawalipwi kabisa katika kazi kama za kulea familia au kuwa mama wa nyumbani

(SAUTI YA PHUMZILE)

image
Mkurugenzi mtendaji wa UN-WOMEN Phumzile Mlambo Ngcuka.(Picha:UM/Rick Bajornas)
“Kimsingi uchumi wote unategemea huduma zisizo na ujira na kazi za nyumbani ambazo mara nyingi hufanywa na wanawake na wasichana, na hivyo aina hii ya kazi huwafanya idadi kubwa ya wanawake na wasicha kuachwa nyuma. Mabadiliko mazuri katika ulimwengu wa kazi yasaidie wanaotoa huduma kuthaminiwa kuanzia kwenye famila. Hii itasaidia kuleta mabadiliko mazuri kuanzia kwa wanawake, jamii na uchumi”

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2015, kutokuwepo kwa usawa kwenye maeneo ya kazi kutaigharimu dunia takriban dola trilioni 12 katika ukuaji wa kiuchumi duniani katika muongo ujao.

Kwa majuma mawili wajumbe watatathimini, kujadili na kutoka na maazimio mbalimbali ambayo yatasaidia mchakato wa kuwawezesha wanawake kufikia ajenda ya 50 kwa 50 ifikapo mwaka 2030 .