Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zaidi zahitajika kukabili umasikini kwa wazee Namibia

Hatua zaidi zahitajika kukabili umasikini kwa wazee Namibia

Namibia imepongezwa kwa ari yake ya kisiasa na mtazamo wa jinsi ya kuboresha maisha ya Wanamibia wote ifikapo 2030 na kulinda haki za binadamu.

Hata hivyo nchi hiyo imetolewa wito wa kutimiza ahadi hizo na mtaalamu huru wa Umoja wa mataifa kuhusu kufurahia haki zote za binadamu kwa wazee Rosa Kornfeld-Matte. Rosa ameihimiza nserikali ya Namibia kuweka juhudi zote zinazohitajika ili kukamilisha na kuweka sera ya kitaifa kuhusu haki, huduma na ulinzi kwa wazee, akisema sera maalumu kuhusu wazee ni muhimu katika kuhakikisha ulinzi na haki kwa watu hao vinaimarika.

Pia amesisitiza kwamba sera yoyote kuhusu wazee ni lazima ichukue mtazamo wa haki za binadamu .Uzee Namibia unaanza kuchukua taswira mpya na barani Afrika unatarajiwa kuongezeka kwa haraka kuliko mabara mingine ilivyokuwa 1950.

Kuna hofu kubwa kuhusu ukatili, dhidi ya wazee, umasikini, njaa na kutothaminiwa hasa miongoni mwa wanawake wazee nchini Namibia na mtaalamu huyo anasema hali hiyo ni lazima ikomeshwe.