Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulizi mawili ya bomu yakatili maisha ya waSyria 40

Mashambulizi mawili ya bomu yakatili maisha ya waSyria 40

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres amelaani mauaji ya watu zaidi ya 40 na kujeruhi wengine katika milipuko miwili ya mabomu yaliyotokea Jumamosi katika mji mkuu wa Syria, Damascus.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa,  wengi wa wale waliouawa walikuwa wasafiri ambao walikuwa wakisafiri kwa basi kwenda katika makaburi takatifu, ambalo hutembelewa zaidi na kundi lingine la kiisilamu lijulikanalo kama Shiite.

Amesema ameshangazwa mno na upuuzwaji wa maisha ya mwanadamu unaonyeshwa na wahalifu, na ametoa wito wa kuwawajibisha waliohusika wa shambulio hilo na mashambulio mengine kama hayo.

Katibu Mkuu ametuma rambirambi zake kwa familia za wahanga na kuwatakia majeruhi afueni ya haraka.