Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Simulizi ya wanawake Afghanistan itabadilika wakishiriki kwenye uongozi - UNAMA

Simulizi ya wanawake Afghanistan itabadilika wakishiriki kwenye uongozi - UNAMA

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao chake kuhusu Afghanistan ambapo mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu nchini humo Tadamichi Yamamoto amesema katika nusu ya kwanza ya kipindi cha serikali ya umoja wa kitaifa, tayari hatua za maendeleo zimepigwa licha ya changamoto zinazotakiwa kupatiwa suluhu siku zijazo.

Ametaja maeneo matatua ambayo yameonyesha matumaini kuwa ni  pamoja na kupambana na rushwa, mchakato wa uchaguzi na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.

Mathalani amesema wakati wa maadhisho ya siku ya wanawake duniani, tarehe nane mwezi huu serikali ilizindua mpango wa kuwapatia kipaumbele wanawake uwezo wa kiuchumi akiongeza kuwa …

(Sauti ya Yamamoto)

"Afghanistan imesalia kuwa ni moja nchi zenye mazingira magumu zaidi kwa mwanamke.  Kwa wanawake wengi, simulizi za ubaguzi, umaskini na ukandamizaji. Kwa simulizi hizo kubadilika, wanawake ni lazima washiriki kikamilifu kwenye uongozi.  Halikadhalika waheshimiwe kama watoa uamuzi kwenye ngazi zote. Hii itahitaji usaidizi thabiti wa serikali ya Afghanistan mashirika ya kiraia na wadau wote wa kimataifa”.

Kuhusu changamoto Bwana Yamamoto ambaye pia ni mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA, ametaja waasi akitaka jumuiya ya kimataifa isaidie nchi hiyo kukabiliana na waasi hao.