Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasichana 20 wauawa baada ya jengo la makazi kuteketea Guatemala

Wasichana 20 wauawa baada ya jengo la makazi kuteketea Guatemala

Nchini Guatemala, wasichana 20 wameteketea kwa moto baada ya jengo lao la makazi kuungua kitendo ambacho kimehuzunisha shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

UNICEF inasema tukio hili la kutisha pia limejeruhi wengine wengi na imeitaka serikali ya Guatemala na na maeneo ya kikanda kuachana na desturi za kuwakusanya watoto na barubaru, ambao ni takriban 240,000 hivi sasa na kuwarundika katika makazi ya malezi ya serikali.

Imetaka serikali izingatie kanuni sahihi za ulinzi wa watoto na imetoa wito wa haraka wa kuunda mfumo wa kitaifa wa ulinzi wa watoto na uongozi utakaohakikisha utekelezaji wake sambamba na mapendekezo ya Kamati ya Haki za Mtoto.

Shirika hilo limetuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga na wananchi na limesema lina imani kuwa serikali ya Guatemala itatimiza wajibu wake wa kuchunguza tukio hilo, kuwatambua wahusika na kutoa fidia kwa waathirika.