Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatari zaidi ya Zika kwa nchi zenye mbu Aedes Aegypti- WHO

Hatari zaidi ya Zika kwa nchi zenye mbu Aedes Aegypti- WHO

Shirika la afya duniani, WHO leo limetoa mwongozo na orodha mpya ya nchi 70 ambazo ziko hatarini kupata maambukizi ya virusi vya Zika.

Mataifa hayo yako katika kanda mbali mbali ikiwemo Ulaya, Amerika, Asia na Afrika ambapo WHO imesema miongoni mwao ni nchi ambako mbu anayeeneza virusi hivyo Aedes Aegypti anapatikana, ingawa maambukizi hayajaripotiwa.

Barani Afrika ni pamoja na Tanzania, Kenya, Rwanda na Malawi ambapo WHO imesema lengo la mwongozo huo si kuzua taharuki bali unalenga kupatia serikali mwelekeo wa kuepusha maambukizi.

Mathalani kwa kuweka ufuatiliaji makini wa mbu na tafiti kuhusu Zika na vifaa vya uchunguzi bila kusahau taarifa za mara kwa mara kwa wasafiri na jamii kuhusu virusi hivyo.

Monika Gehner ni afisa kutoka WHO na anaeleza ni kwa jinsi gani taarifa hizi mpya zitasaidia.

(Sauti ya Monika)

Hii itatusaidia kwa sababu sasa tunaweza kutathmini hatari ya Zika kwa uhakika zaidi. Kwa sababu hata kama unafahamu hakuna maambukizi ya Zika lakini kuna mbua aina ya Aedes aegypti basi uko hatarini kupata maambukizi hasa wakati huu ambapo kuna wasafiri wengi wa kimataifa. Kwa hiyo kama msafiri mmoja mwenye virusi vya Zika anaweza kwenda kwenye nchi yenye mbu huyo, na hao mmbu wanaweza kueneza kwa watu wengine na huo ndio mzunguko wa maambukizi.”

Hadi sasa matumaini yanaendelea huenda penginepo chanjo dhidi ya virusi vya Zika inaweza kupatikana.